Rais wa Jamhuri ya Zimbabwe Mhe. Emmerson Dambudzo Mnangagwa tayari amemaliza ziara yake rasmi ya kiserikali ya siku mbili nchini Tanzania, Rais John Pombe Magufuli ambaye alikuwa mwenyeji wake amemsindikiza katika viwanja vya ndege vya Mwalimu Julias Kambarage Nyerere tayari kurejea nchini kwake.

Ujio wa Rais huyo umejikita katika mambo matatu ambayo Rais Magufuli ameyasema pindi alipoongea na waandishi wa habari Ikuli jijini Dar es salaam, ambapo amesema wamezungumza jinsi ya kuimarisha uchumi wa nchi hizi mbili kiuchumi tofauti na uhusiano wa zamani uliokuwa wa kisiasa zaidi.

Pia wamekubaliana kupitia jumuiya ya Ushirikisho wa Nchi za Kusini mwa Afrika (Sadc), kukuza biashara ambapo amesema ipo mikataba mbalimbali ya kulegeza masharti ya kibiashara katika Sadc.

Rais Mafuli ameongezea kuwa wamekubaliana kukuza uwekezaji ambapo watashirikiana kutumia kwa wingi vivuto vilivyopo hapa nchini.

Aidha Rais Mnangagwa ametoa shukrani za dhati kwa wenyeji wake kwa kumpokea vizuri.

 

Prof. Jay awekwa kikaangoni, atakiwa kutoa ushahidi
Hamisa Mobeto: Sina haja ya kulalamika, sikupanga njia yangu iwe hii