Rais wa Zimbabwe, Emmerson Mnangagwa amewasili nchini Tanzania katika ziara ya kwanza tangu aingie madarakani.

Ni ziara ya siku mbili ambayo imelenga kuimarisha uhusiano wa Kidiplomasia kati ya mataifa hayo mawili kwa mujibu wa wizara ya mambo ya nje.

Aidha, amewasili asubuhi na kupokelewa na mwenyeji wake Rais Dkt. John Pombe Magufuli katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

Kiongozi huyo anatarajiwa kutembelea chuo cha kilimo alikosomea na miongoni mwa wapigania uhuru waliotoka nchi za kusini mwa Afrika.

Hata hivyo, Rais Magufuli alikuwa miongoni mwa viongozi wa Afrika waliompongeza Rais Mnangagwa kwa kuchukua uongozi wa nchi pasi kushuhudia ghasia za aina yoyote.

 

Chid Benz asakwa kwa Deffender
Askofu mwenye watoto 149 afungwa, ana wake 24