Rais wa Shirikisho la Soka Duniani (FIFA), Gianni Infantino ameanza kuandamwa na mzimu wa kashfa ya rushwa uliomuondoa mtangulizi wake, Joseph ‘Sepp’ Blatter.

Kwa mujibu wa nyaraka zilizotolewa na gazeti la Panama, Infantino anahusishwa na dili lenye harufu ya rushwa kati ya kampuni moja na Uefa inayosimamia mpira wa miguu barani Ulaya, lililokamilishwa wakati akiwa Mkurugenzi wa Idara ya Sheria ya Uefa.

Kwa mujibu wa nyaraka hizo, dili hilo lilokamilishwa kati ya mwaka  2003 na 2006 zilisainiwa pia na Inflantino na linaihusisha Uefa kwa mara ya kwanza na moja kati ya makampuni yaliyohusika katika kashfa nzito zilizomuangisha mtangulizi wake, Sepp Blatter.

Hata hivyo, Infantino amekanusha vikali kashfa hizo alizodai zinalenga katika kumchafulia jina lake na heshima yake na kwamba hatakubaliana na hali inayotaka kumtia dosari. Kadhalika,  Uefa wamekanusha vikali kuhusika wala afisa wake yoyote kuhusika na dili hilo.

 

Al Ahly Yawasili Dar es salaam, Wajifanya Mabubu
Rais Zuma anusurika Bungeni