Rais Mstaafu wa Ufaransa, Nicolas Sarkozy anashikiliwa na polisi akihojiwa kuhusu tuhuma za kupokea fedha za kufadhili kampeni zake kutoka kwa kiongozi wa zamani wa Libya Kanali, Muammar Gaddafi.

Polisi wanachunguza tuhuma hizo kuhusiana na ufadhili wa fedha hizo alizotumia kwenye kampeni za uchaguzi wa urais mwaka 2007.

Aidha, Msaidizi wa Rais huyo wa zamani wa Ufaransa, Alexandre Djouhri pia alikamatwa jijini London hivi karibuni kwa ajili ya uchunguzi.

Hata hivyo, Sarkozy alishindwa katika juhudi zake za kutaka kurejea madarakani mwaka 2012

Waandamanaji 47 wauawa wakimpinga Rais Kabila
Yanga yamsubiri kwa hamu mpinzani wake