Baada ya miaka 30, hatimaye, rais mstaafu wa awamu ya pili ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Alhaj Ali Hassan Mwinyi ametengua kauli yake juu ya soka la Tanzania.

Mzee Mwinyi ambaye alikuwa mgeni rasmi katika mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika (CAF), kati ya Simba dhidi ya Gendarmerie ulioshuhudiwa Simba ikipata ushindi wa mabao 4-0.

Mzee Mwinyi alivutiwa na soka la Simba lililoonyeshwa kwenye mchezo huo na baada ya mechi alifuta kauli yake aliyoitoa miaka 30 iliyopita aliposema “Tanzania ni kichwa cha mwendawazimu” .

Akizungumza baada ya mchezo huo wa jana uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa, Mzee Mwinyi alisema:

“Nimeshuhudia mchezo mzuri na sasa nafuta lile neno kwamba Tanzania ni kichwa cha mwendawazimu kila anaetaka kujifunza kunyoa atunyoe sisi, sasa nyie ndio vinyozi.”

Jafo awataka Maafisa utumishi kujitathmini
Rais afanya uteuzi mwingine