Rais mstaafu wa Mauritania, Mohamed Ould Abdel Aziz (66), atafikishwa mahakamani hapo kesho Januari 26, 2023, ikiwa ni tukio nadra la kiongozi wa zamani wa nchi barani Afrika kufikishwa mahakamani.

Kiongozi huyo mstaafu ambaye ni Jenerali wa zamani, anakabiliwa na mashitaka ya kujikusanyia mali kinyume cha sheria wakati wa utawala wake wa miaka 11 baada ya kuingia madarakani kwa mapinduzi.

Rais wa zamani wa Mauritania Mohamed Ould Abdel Aziz. Picha ya Ludovic Marin/AP

Abdel Aziz, alijiuzulu mwaka wa 2019 baada ya mihula miwili ya urais ambapo aliuangamiza uasi wa itikadi kali, uliokuwa unatishia taifa hilo huku yeye na vigogo wengine 11 kutoka utawala wake wa zamani wakishitakiwa kwa tuhuma za rushwa, utakatishaji fedha na kujikusanyia mali kinyume cha sheria.

Washitakiwa hao, wanajumuisha mmoja wa wakwe zake, mawaziri wakuu wawili wa zamani na mawawiri kadhaa wa zamani na wafanyabiashara, ambapo hata hivyo Abdel Aziz alikataa kujibu maswali, kuhusu chanzo cha utajiri wake.

Serikali haitaki kusikia Wananchi wakilalamikia umeme: Makamba
Baleke anaitaka Ligi ya Mabingwa Afrika