Rais Mstaafu wa Nigeria, Olusegun Obasanjo amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli kwa kuonyesha mfano bora barani Afrika katika kusimamia uchumi na kutetea maslahi ya nchi.

Obasanjo ametoa pongezi hizo mapema hii leo mara baada ya kukutana na Rais Magufuli Ikulu Jijini Dar es salaam na kufanya mazungumzo, ambapo amesifu jitihada za Rais huyo za kuwakaribisha wawekezaji na wafanyabiashara kutoka sehemu mbalimbali duniani na kusimamia vizuri sera kuhakikisha nchi inanufaika.

“Uchumi wa Tanzania unakuwa kwa kasi kubwa, na juhudi ya Rais ya kuhakikisha nchi inanufaika na uwekezaji kitu ambacho ni suala mhimu sana na ameonyesha mfano wa kuigwa kwa bara zima la Afrika, na hii ndio njia sahihi ya kuweza kuinua uchumi wetu, hatuwezi kuendelea kuona wananufaika wao halafu sisi tunaambulia kidogo,”amesema Obasanjo.

Hata hivyo, ameongeza kuwa amepita katika nchi kadhaa zikiwemo Msumbiji, Malawi na sasa yupo hapa Tanzania na huko kote amekuwa akizungumzia masuala ya uchumi na uwekezaji barani Afrika.

Watakaosajiliwa Njombe Mji FC Wapatikana
Mourinho atuhumiwa kukwepa kodi Uhispania