Aliyekuwa Rais wa nchi ya Ureno, Mario Soares katika kipindi cha kuanzia mwaka 1986 hadi mwaka 1996 amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 92.

Mario Soares anaheshimika kama baba wa demokrasia nchini humo na ndiye mwanzilishi wa chama cha kisosholisiti nchini humo, pia rais huyo katika kipindi cha uhai wake alitumia miongo kadhaa katika masuala ya siasa ikiwa ni pamoja na kuwa mstari wa mbele wakati wa mchakato wa nchi hiyo kujiunga kwenye Umoja wa Ulaya.

Soares alikuwa rais wa nchi hiyo baada ya kuwa tayari amelitumikia taifa hilo katika nyadhifa za uwaziri wa mambo ya nchi za nje na Waziri Mkuu.

Kufuatia kifo cha rais huyo mstaafu, Ureno imetangaza siku tatu za maombolezo kuanzia Jumatatu kwa ajili ya kuomboleza kifo cha kiongozi huyo.

Majaliwa awasweka ndani maafisa wanne Masasi
Gambo kumaliza migogoro yote Arusha