Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe, ametaka kurudishwa kwa hukumu ya kifo nchini mwake kwani watu wanacheza na maisha ya watu kwa kuua wenzao.

Mugabe ametoa taarifa hiyo alipokuwa kwenye mazishi ya mwanasiasa mwenzake mjini Harare, na kusema kuwa sheria ya kunyongwa irudishwe kwani watu wanacheza na kifo kwa kuua wenzao.

“Acha turudishe hukumu ya kifo, watu wanacheza na kifo kwa kuua wenzao, hivi hii ndio sababu ya kuikomboa nchi? Tunataka nchi hii iwe ya amani na furaha, sio nchi ambayo watu wanauana,” amesema Rais Mugabe

Aidha, taarifa zimeendelea kueleza kuwa kauli hiyo imekuja kufuatia taarifa ya Waziri wa Sheria kusema kuwa zaidi ya watu 50 wameomba nafasi ya kazi ya kunyonga watu mwezi uliopita.

Hata hivyo, tukio la mwisho la kunyongwa mtu hadi kufa nchini humo lilikuwa mwaka 2005 baada ya mtu aliyekuwa akifanya kazi ya kunyonga kustaafu, ambapo mpaka sasa zaidi ya wafungwa 90 wapo wanasubiri hukumu ya kifo.

MCT kuwashugulikia wanaowanyanyasa waandishi wa habari
James Collins aibwaga Wales, Chris Coleman asikitika