Rais wa Uganda, Yoweri Museven amepingwa vikali na Wabunge wa Bunge la Uganda dhidi ya ombi lake la kutaka kuongezewa washauri wake binafsi huku wakisema kufanya hivyo kutasababisha matumizi mabaya ya fedha.

Wabunge  hao wamesema kuwa fedha ambazo zitatumika kuwalipa washauri hao zinaweza kutumiwa kwa kununua vifaa vya hospitali na kuongeza mishahara ya madaktari.

Kwa mujibu wa gazeti la Obsever, inadaiwa kuwa Rais Museveni ametoa ombi la kuongeza washauri 18 hivyo kuwa na jumla ya washauri 163.

Aidha, Gazeti hilo limeripoti kuwa imekuwa ni kawaida na utamaduni kwa rais Museveni kuongeza washauri baada ya uchaguzi wa urais ama baada ya kufanya mabadiliko ya baraza lake la mawaziri.

Hata hivyo, kila mshauri atakakae chaguliwa atakuwa anapokea mshahara wa dola 631 pamoja na dereva atakayelipwa dola 53.

Young Africans Kuondoka Dar es salaam Leo
Serengeti Boys Kuifuata Cameroon