Waganda wafanya majadiliano ya kuhoji katika mitandao ya kijamii ni simu gani ya dharura aliyoipata Rais wao Yoweri Museveni mpaka kupelekea kusimamisha msafara wake kijiji kimoja mpakani na Tanzania.

Picha zinazosambaa mitandaoni  zinaonyesha kuwa Rais Museven alishuka kutoka kwenye gari na kuketi kwenye kiti chake alichokiweka  kando kando ya barabara mpya ya Isingiro ikipitia kijiji hicho cha Kyeirumba hadi Tanzania na kupokea simu ya faragha

Hata hivyo museveni akiwa kando ya barabara alifanya shughuli hiyo ya kuongea na simu huku akiwapungia mikono wapita njia.mu7

Aidha baadhi ya  maswali yaliyokuwa yakiendelea mitandaoni ni kama haya hapa chini na wengine wakidhani ya kuwa ni kuhusu kuachiwa kwa kiongozi wa upinzani Kizza Besigye

”kwani asingeweza kupokea simu yake ndani ya gari lake ?

”ni siri gani hiyo ambayo hakutaka hata walinzi wake wasikie,

”Ama ilikuwa ni #Besigyexit ? wakizungumzia kuachiliwa kwa dhamana kwa kiongozi wa upinzani Kizza Besigye.

Waziri Mkuu, Majaliwa Atoa Wito kwa Wakurugenzi
Ndoa Ya TFF Na Azam Media Ltd Yaimarishwa