Rais wa Uganda, Yoweri Museveni amewapa Kanye West na Kim Kardashian majina ya Kiganda, kama sehemu ya zawadi yake kwao.

Rais Museveni ambaye alipokea zawadi ya kiatu cheupe kutoka kwa familia ya Kanye West aliyokutana nayo Ikulu, amesema kuwa amembatiza Kanye West jina la ‘Kanyesigwe’ linalomaanisha ‘Naamini’.

Rais huyo ambaye aliwahi kutunga shairi la rap miaka kadhaa iliyopita, amesema kuwa amempa Kim Kardashian jina la ‘Kemigisha’, linalomaanisha ‘mwenye baraka kutoka kwa Mungu’.

Taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Rais, imeeleza kuwa wawili hao walionesha kufurahishwa na majina hayo waliyopewa na Rais Museveni.

“Hapa ni chanzo cha maisha ya binadamu, hata watu weupe asili yao ilianzia hapa [Afrika],” Rais Museveni anakaririwa kwenye taarifa hiyo.

Melanini, mtoto wa kike wa Rais Museveni akiwa na Kanye West na Kim Kardashian

Kanye West ambaye mwezi uliopita alitaka kuanza kufahamika kama ‘Ye’, amesema kuwa wamefurahi kuwa Uganda ambapo amepataja kama ‘nyumbani’.

Rapa huyo ameingia nchini Uganda kukamilisha azma yake ya kurekodi albam yake mpya barani Afrika, na tayari ameshaanza kazi hiyo nchini humo.

Chadema yakanusha Mbowe na Mashinji kutofautiana
Habari kubwa katika magazeti ya Tanzania leo Oktoba 16, 2018

Comments

comments