Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi ameitaka Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makaazi kuwa na mipango bora ya matumizi ya ardhi itakayobainisha maeneo yaliotengwa kwa ajili ya makaazi pamoja na yale ya ibada.

Ameyasema hayo leo katika mkutano wa viongozi wa Dini ya kikiristo uliowahusisha Maaskofu, Wachungaji na waumini wa madhehebu mbalimbali wa dini hiyo, ukiwa na lengo la kuwashukuru baada ya kumchagua kwa kishindo katika uchaguzi mkuu uliopita, sambamba na kusikiliza changamoto zinazowakabili.

Rais Mwinyi amesema kuwepo kwa mipango bora katika matumizi ya Ardhi kutaondoa changamoto zinazojitokeza za kufanyika ujenzi wa holela wa nyumba za Ibada, ambapo waumini wa dini tofauti hujenga majengo yao katika eneo moja.

Aidha, Dkt. Mwinyi amewataka watendaji wanaoshughulikia utoaji wa vibali vya kazi nchini, kuondokana na urasimu pamoja na utozaji wa gharama kubwa kwa watumishi wa Dini wanaotoka nje na kuja nchini kwa njia ya kujitolea.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti a Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi akisalimiana na Viongozi wa Dini ya Kikristo  alipowasili katika viwanja vya Ukumbi wa Amani Utengamano Welezo Mjini  Zanzibar kwa ajili ya Mkutano wa Viongozi hao uliofanyika leo.[Picha na Ikulu] 29/09/2021.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti a Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi (kulia) akiteta na baadhi  ya Viongozi wa Dini ya Kikristo   kabla  ya Mkutano wa Viongozi hao uliofanyika leo   katika Ofisi ya Ukumbi wa Amani Utengamano Welezo Mjini  Zanzibar.[Picha na Ikulu] 29/09/2021.
Baadhi ya Masister na Viongozi wengine wa Madhehebu ya Dini ya Kikristo ni miongoni mwa washiriki wa mkutano wa Viongozi hao uliofanyika leo katika Ukumbi wa Amani Utengamano Welezo Mjini  Zanzibar mgeni rasmi alikuwa rais wa Zanzibar na mwenyekiti wa Baraza la mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi.[Picha na Ikulu] 29/09/2021.

Try Again akubali kumrithi Mo Dewji
RC Makalla atangaza Dar Sunset Carnival Coco Beach