Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi amekutana na Balozi mdogo wa India Zanzibar Dkt. Kumar Praveen aliyefika Ikulu kujitambulisha.

Mazungumzo yao, yamegusia masuala kadhaa muhimu ikiwemo Miradi ya Maji safi na salama Zanzibar, wamejadili Chuo cha Ufundi na Amali Pemba kinachotoa mafunzo ya ufundi na ujuzi kwa vijana.

Aidha, wamezungumzia ufadhili wa masomo kutoka India ikiwa ni fursa za ufadhili wa masomo kwa wanafunzi kutoka Zanzibar kwenda India kusoma katika vyuo au taasisi za elimu ya juu.

Rais Dk Mwinyi ameishukuru Serikali ya India kwa ushirikiano na ufadhili wa Miradi ya maji ambayo inatekelezwa kupitia mkopo wa Benki ya Exim India.

Aidha, Balozi Mdogo Dkt. Kumar Praveen amemweleza Rais Dkt. Mwinyi kuhusu ujio wa Waziri wa Mambo ya nje wa India, Dkt. Subrahmanyam Jaishankar Julai 2023 kwa ajili ya uzinduzi wa Miradi ya Maji Zanzibar.

NEMC iwachukulie hatua wanaotiririsha maji machafu - Ndejembi
Vifungashio vya plastiki chachu uchafuzi wa mazingira - Serikali