Rais wa Bolivia, Evo Morales ametangaza kujiuzulu kupitia hatuba yake na runinga.

Uamuzi huo umekuja muda mchache baada ya uchunguzi uliofanywa na OAS juu ya matokeo ya uchaguzi wake ambao ulitangaza kuwa mshindi mwezi uliyopita kugubikwa na udanganyifu.

Evo Morales ametangaza hatua hiyo siku ya Jumapili kwamba amewasilisha barua yake ya kujiuzulu bungeni baada ya jeshi, polisi na upinzani kumtaka kufanya hivyo.

“Matamanio yetu makubwa ni kuona amani inarejea kwa watu wetu,” amesema Morales katika runinga wakati huo huo makamu wake wa urais Alvaro Garcia Linera naye akitangaza kujiuzulu kwake.

“Ninaomba kuacha kushambuliana, kuacha kuchoma vitu na kushambuliana,” Morales alipowaambia watu wa Bolivian.

Rais huyo amenukuliwa akisema kwamba ameamua kuitisha uchaguzi mwengine ili wananchi wa Bolivia waweze kuchagua serikali mpya kwa njia ya kidemokrasia.

Kwa wiki kadhaa Bolivia imeshuhudia machafuko na ghasia dhidi ya madai ya udanganyifu katika uchaguzi wa Oktoba 20nambapo watu watatu wameuawa na zaidi ya 300 kujeruhiwa.

Matokeo ya uchaguzi uliopita yalimpa ushindi Morales kwa asilimia 10 dhidi ya mpinzani wake Carlos Mesa. Upande wa upinzani umeishutumu serikali kwa udanganyifu.

Adama Traore aikacha Mali, kuziba nafasi ya Moreno
Rais wa Bolivia ajiuzulu, Atangaza uchaguzi Mpya