Bashir pia amezivunja serikali za mitaa na taifa na ameahidi kuunda serikali mpya baada ya mjadala wa kitaifa kufanyika huku wakati huo huo maandamano yakiendelea nchini humo.

“Natoa wito kwa bunge kuchelewesha mchakato wa kurekebisha katiba kwa ajili ya kufungua milango ya kuimarisha hali ya kisiasa kupitia mijadala yenye kujenga taifa na kuchukua hatua za kweli za kizalendo,” amesema Bashir katika hotuba yake

Uamuzi huo umekuja baada ya miezi miwili ya maandamano nchini humo yaliyosababishwa na hali mbaya ya uchumi na kuongezeka kwa bei za bidhaa, iliyopelekea kuwepo kwa shinikizo la rais wa nchi hiyo, mwenye umri wa miaka 75 kujiuzulu.

Aidha, Omer Ismail, mshauri wa ngazi ya juu katika mradi wa Washington-based Enough Project amesema kuwa Bashir ametangaza hali ya dharura ya Taifa ili aweze kutangaza sheria ya kijeshi, inayompa rais amri ya kufanya maamuzi binafsi.

Hata hivyo, nchini Sudan kumekuwa na maandamano yaliyodumu tangu Disemba 19 mwaka jana, baada ya serikali ya nchi hiyo kupandisha bei ya chakula.

 

EWURA kuanzisha vituo vya mafuta vinavyotembea
Baada ya kushushiwa kipigo kutoka kwa Simba, Yanga na Azam FC kushuka dimbani tena