Rais wa Urusi, Vladimir Putin ameusifu mpango wa China wa kuimarisha miundombinu akitilia mkazo mahusiano mazuri yaliyopo kati ya mataifa hayo yenye nguvu.

Putin ameyasema hayo kwenye mkutano uliohudhuriwa na viongozi zaidi ya 40 jijini Beijing ambapo amesema kuwa mpango huo wa China unalenga kuimarisha ushirikiano wa mataifa ya Ulaya na bara Asia.

Aidha, matamshi hayo yanaashiria kuondoa uwezekano wa kuzuka mivutano kati ya Urusi na China na mshikamano wa pamoja wa mataifa hayo dhidi ya ushawishi wa Marekani duniani.

Hata hivyo, mpango huo wa kufadhili barabara na miundombinu mingine unaojulikana kama Belt and Road tayari umetanua ushawishi wa kiuchumi wa China kwenye kanda ya Asia ya Kati eneo ambalo Urusi imekuwa na ushawishi wake kwa muda mrefu.

Video: Rais Magufuli aingilia kati usajili laini kwa vidole, Kimbunga Keneth chayeyuka
Dkt. Bashiru afunguka kuhusu Lowassa, ' Huyu ilibidi akubalike kwanza kwenye tawi'