Rais wa Urusi, Vladimir Putin amewasili nchini China na kukutana na rais, Xi Jinping katika ziara ya siku tatu yenye lengo la kuimarisha ushirikiano wa kijeshi na kiuchumi kwa nchi hizo mbili.

Rais wa China Xi Jinping amemkaribisha rais Putin kwa gwaride la heshima katika ukumbi wa kitaifa uliopo jijini Beijing.

Aidha, Viongozi hao wote wawili hawakualikwa katika mkutano wa kilele wa mataifa saba yenye nguvu za kiuchumi na biashara duniani G7 unaofanyika nchini Canada.

Hata hivyo, katika mahojiano yaliyofanywa na chombo kimoja cha habari cha China, Putin amesema kuwa Urusi na China wana nia ya kuimarisha ushirikiano wao katika maeneo kama miundombinu, nishati, utafiti wa kisayansi na masuala ya teknolojia ya hali ya juu.

 

Magazeti ya ndani na nje ya Tanzania leo Juni 10, 2018
Video: Mkuchika kula sahani moja na wanaokwamisha mafao