Kutokana na machafuko yaliyozuka nchini Afrika Kusini Rais wa nchi hiyo, Cyril Ramaphosa hatahudhuria mkutano mkuu wa umoja wa mataifa jijini New York, baadae mwezi huu badala yake, amesema atabaki nchini humo kushughulikia changamoto zinazokabili nchi yake.

Kwa mujibu wa BBC Rais wa Afrika kusini Ramaphosa ameahidi msururu wa hatua kukabiliana na mzozo ikiwemo kuidhinisha daftari la wahalifu, kuongeza idadi ya mahakama maalum ya wahalifu wa unyanyasaji wa kingono na hukumu kali zaidi.

Vitendo vya mashambulizi ya chuki dhidi ya raia wa kigeni na unyanyasaji dhidi ya wanawake vimeibua hisia kali kwa mataifa mengine ya Afrika na kupelekea siku ya Ijumaa, mamia ya wanawake, ambao walikuwa wamevaa mavazi ya rangi nyeusi, kuanza kukusanyika Johannesburg saa za asubuhi ili kuongeza uelewa dhidi ya dhuluma ya kijinsia.

Takwimu za hivi karibuni za uhalifu, ambazo zilitolewa Alhamisi, zilidhihirisha kwamba hofu yao ni dhahiri, mauaji, ubakaji na unyanyasaji wa kijinsia vimeongezeka.

Wauaji waliorekodiwa na polisi wamekuwa wakiongezeka kila mwaka kwa muongo mmoja uliopita, na makosa ya unyanyasaji wa kijinsia ikiwemo ubakaji yameongezeka kwa asilimia 4.6 mwaka huu.

Kutolewa kwa takwimu hizo kunakuja huku kukiwa na wasiwasi mkubwa kuhusu dhuluma dhidi ya wanawake baada ya visa vingi vya ubakaji na mauaji katika wiki chache zilizopita.

Aidha waafrika kusini wameghadhabishwa na msururu wa visa vya ubakaji na mauaji ya wanawake katika wiki za hivi karibuni, kikiwemo cha msichana wa shule aliyevunjwa fuvu la kichwa na mwanafunzi wa chuo kikuu aliyepigwa kwa kifaa butu hadi kufariki.

Hata hivyo ubakaji na mauaji yamechangia maandamano na kampeni ya #AmINext campaign katika mtandao wa kijamii Twitter, na waraka uliotiwa saini na zaidi ya watu 500,000 kutaka kurudishwa kwa hukumu ya kifo katika taifa linalokabiliana na viwango vya juu vya uhalifu.

Polepole amuagiza mkurugenzi kuwatengea mamilioni vijana na wanawake
Kurasa za WhatsApp kuanza kurusha matangazo 2020