Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan amefanya mabadiliko madogo ya Baraza la Mawaziri kwa kumteua Jenista Mhagama kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu).

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya Habari na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Zuhura Yunus hii leo Aprili Mosi, 2023 imesema Mhagama anachukua nafasi ya George Boniface Simbachawene na kabla ya uteuzi huo alikuwa ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora.

Aidha, Rais Samia pia amemteua George Boniface Simbachawene kuwa Waziri wa
Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, akichukua  nafasi ya  Jenista Mhagama ambapo kabla ya uteuzi huo Simbachawene alikuwa Waziri wa Nchi,
Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu).

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, teuzi huo umeanza Aprili Mosi, 2023 na Mawaziri wateule wataapishwa Aprili 2, 2023 Ikulu, jijini Dar es Salaam.

Habari Kuu kwenye magazeti ya leo April 2, 2023
Tiba mbadala: Dawa kwa wanaosumbuliwa na Kisukari