Rais Samia Suluhu Hassan hii leo Julai 8 ametoa Mabadiliko madogo ya baraza la mawaziri, Makatibu wakuu na Naibu makatibu wakuu.

Akisoma mabadiliko hayo mbele ya waandishi wa habari Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Hussein Kattanga amesema Rais amefanya mabadiliko ya muundo katika wizara tatu.

Rais Samia amebadilisha Wizara ya Uwekezaji iliyokua chini ya waziri Mkuu ikaungana na Wizara ya Viwanda na Biashara ambayo itaitwa Uwekezaji, Viwanda na Biashara.

Ameunda wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi maalumu. na pia amefanya mabadiliko katika wizara ya Afya.

Katika uteuzi wa mawaziri, Nape Moses Nnauye amekuwa Waziri wa Habari, Mawasiliani na Teknolojia ya Habari, pia Hamad Masauni kuwa Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, amemteua Dkt Pindi Chana kuwa Waziri katika Ofisi ya waziri mkuu atakaeshughulikia Sera, Bunge na Uratibu. Pia amemteua Dkt Angelina Mabula kuwa waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Hussein Bashe atakuwa Waziri kamili wa Kilimo.

Manaibu waziri watano, Antony Peter Mavunde atakuwa Naibu Waziri wa Kilimo, Jummanne Abdallah Sagini Naibu waziri wa Mambo ya Ndani, Dtk Lemomo Ole Naibu waziri wizara ya Madini, Ridhwani Kikwete kuwa Naibu Waziri wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, na Atupele Fred Mwakibete kuwa Naibu Waziri wa Ujenzi.

Pia Rais Samia amebadilisha Mawaziri 9 kutoka wizara walizokuwa wakihudumu mwanzo na Manaibu waziri watatu kutoka wizara walizokuwa wakihudumu mwanzo, na kubadilisha makatibu wakuu na manaibu makatibu wakuu.

Hivi karibuni katika hotuba yake mbele ya viongozi wa Serikali Ikulu alipokua akipokea taarifa ya utekelezaji wa mpango wa maendeleo wa Fedha za Uviko 19 Rais Samia alisema atafanya mabadiliko ya baraza la Mawaziri kutokana na kili alichotaja kuwa baadhi ya waliokuwa katika baraza hawakuwa njia moja na yeye.

Habari kubwa kwenye magazeti leo, Januari 9, 2022
Afisa wa polisi akatisha uhai wake