Rais Samia Suluhu Hassan amekutana na kuzungumza na Makamu wa Rais wa Marekani, Kamala D. Harris, leo Aprili 15, 2022 nchini Marekani.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akiwa na Mwenyeji wake Makamu wa Rais wa Marekani Mhe. Kamala Harris wakati wakizungumza na Wanahabari katika Ikulu ya Marekani White HouseWashington leo tarehe 15 Aprili, 2022.

Katika Mazungumzo yao Rais Samia ametaja nia na madhumuni ya kufika Nchini Marekani kuwa ni kufanya Uzinduzi wa Filamu maalumu inayoangazia Maeneo ya Utalii nchini Tanzania “The Royal Tour”.

Rais Samia amesema kuwa Marekani ni moja ya nchi kuu ulimwenguni ambapo starehe na Mapumziko ya wanadamu huchukuliwa kwa umuhimu ndio sababu mojawapo ya kuchagua Nchi hiyo iwe katika zile zitakazohusika kuzindua Filamu hiyo. Kwa Upande wake Makamu wa Rais wa Marekani, Kamala D. Harris amesema Marekani iko tayari kuendeleza ushirikiano na Tanzania na Nchi zote za Afrika.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akiongoza Ujumbe wa Tanzania katika Mazungumzo Rasmi na Ujumbe wa Serikali ya Marekani ulioongozwa na Makamu wa Rais wa Marekani Mhe. Kamala Harris katika Ikulu ya White House Washington leo tarehe 15 Aprili, 2022.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akizungumza jambo na Mwenyeji wake Makamu wa Rais wa Marekani Mhe. Kamala Harris wakati akiangalia mandhari ya Majengo ya Ofisi za Ikulu ya Marekani mara baada ya kuzungumza na Wanahabari katika Ikulu hiyo ya White House Washington leo tarehe 15 Aprili, 2022.

Muaddi afunguka ya Rihanna na Baba mtoto wake
Mzamiru: Hatma ya Simba ni Jumapili