Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi wa viongozi mbalimbali, amemteua Mcha Hassa Mcha kuwa Naibu Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA.

Aidha kabla ya uteuzi Mcha alikuwa Kamishna wa Udhiniti na Utekelezaji Makao makuu ya Mamlaka Mapato Tanzania TRA, Mcha anachukua nafasi ya Msafiri Lameck Mbibo ambaye ameteuliwa kuwa Naibu Katibu Wizara ya Madini.

Aidha utezi huo umeanza Desemba 5, 2021

Aidha Rais Samia amemteua Balozi Celestine Josph Mushy kuwa Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Austria.

Balozi Mushy alikuwa Katibu Tawala Msaidizi Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara, ambapo uteuzi huo umeanza Januari 14, 2022.

Bocco: Kufunga ni mipango ya Mungu
Kocha Pablo amkingia kifua Bocco