Rais Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi wa viongozi mbalimbali akiwamo Jaji Mkuu Mstaafu Mohammed Chande Othamn aliyeteuliwa kuwa Mkuu wa Chuo Kikuu cha cha Ardhi (ARU).

Taarifa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu Jaffar Haniu imesema Rais Samia amemteua Profesa Elisante Ole Gabriel kuwa Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania. Kabla ya uteuzi huu Profesa Ole Gabriel alikuwa Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi.

Uganda kuwapokea wakimbizi 2000 wa Afganistan
Rais Joe Biden atetea uamuzi wake