Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amesema Bara la Afrika linahitaji kuongeza juhudi zaidi kwa kufanya jitihada mbalimbali zitakazoendeleza mchezo wa Soka.

Kauli hiyo imetolewa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa leo Agosti 10, 2022 alipomuwakilisha Mheshimiwa Rais Samia katika ufunguzi wa Mkutano wa 44 wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) jijini Arusha.

“Rais Samia aliamua na kukubali kuwa mdhamini wa mashindano ya Klabu Bingwa kwa vilabu vya Nchi za Afrika Mashariki na Kati (SAMIA CUP) ili kuunga mkono maendeleo ya mpira wa miguu Afrika na duniani.”

Mheshimiwa Majaliwa amesema Rais Samia anaamini mkutano huo utafungua njia kwa Tanzania kuwa mwenyeji wa mikutano mingine ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Duniani (FIFA) na CAF na kutoa fursa ya kuandaa mashindano mbalimbali yanayoandaliwa na CAF na hata FIFA.

Joto la matokeo ya uchaguzi Kenya lazidi kupanda
Mabilioni yamwagwa mikopo ya vijana