Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, ameelezea namna ambavyo Mama Anna Mkapa alimshawishi kuingia katika siasa, na ndipo safari yake ya siasa ilipoanza.

Rais Samia amesema hayo wakati wa Sherehe ya miaka 25 tangu kuanzishwa kwa Mfuko wa Fursa sawa kwa wote ambao unasimamiwa na mama Anna Mkapa.

“Nakumbuka siku moja tulikuwa tunakwenda kuwatembelea wakina Rugimbana kijijini kwao Chamanzi, kulikuwa na kijiji cha vijana na wakati watu wote wanaingia kwenye magari mimi nilikuwa nimezubaa… Mama alikuwa kwenye gari akaniona nimezubaa akaniuliza wewe Mpemba vipi nikamwambia magari yamenikimbia akaniambia ingia humu,” amesema Rais Samia.

Rais Samia ameongeza, “Wakati niko kwenye gari akaniambia wewe unafaa uingie kwenye siasa, nikamwambia naanzia wapi akasema niulize wenzangu wameingiaje na ndipo mwaka 2000 nikaingia Baraza la Wawakilishi na baadaye Waziri, Makamu wa Rais na sasa niko hapa,”

“Hapa kuna watu wametoa ushuhuda na mimi nataka nitoe wangu. Mimi mwenzenu nilijiunga na EOTF mwaka 1997 nikiwa kama mmoja wa Bodi ya Wadhamini nikiwa kijana kisichana machachari sana lakini nilipata breki yangu Mama Mkwizu ndiye aliyenishika mkono akaniambia wewe tulia hapa.”

Nilifanya kazi pamoja na Bodi kwa miaka mitatu hadi 2000 nikaingia mambo ya siasa, na iliyoniingiza kwenye siasa ni hiyo EOTF.



Sakho awatuliza Simba SC, aahidi makubwa 2022/23
Rally Bwalya: Nilitamani kucheza Afrika Kusini