Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amemteua Prof. Mark Mwandosya kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na maji (EWURA).

Taarifa ya uteuzi huo, imetolewa hii leo Agosti 19, 2022 na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Zuhura Yunus ambaye amesema uteuzi wa Mwandosya umeanza Agosti 15 mwaka huu.

Mwandosya ambaye pia aliwahi kushika nyadhifa mbalimbali Serikalini ikiwemo uwaziri katika Wizara mbalimbali, anashika nafasi ya Prof. Jamidu Hazzam ambaye muda wake umemalizika.

Kenya: Ugeni 'wamlazimisha' Kenyatta kuongea
Mkuu wa Mkoa asitisha matumizi ya vifungashio vya plastiki