Rais Samia Suluhu Hassan leo Januari 4, 2021 ameendelea kusisitiza juu ya umuhimu wa mikopo kwa nchi na maendeleo ya wananchi, Ikulu jijini Dar es Salaam mbele ya Viongozi wa serikali wakati wa kupokea taarifa ya utekelezaji wa Mpango wa Maendeleo kwa Ustawi wa Taifa na Mapambano dhidi ya Uviko-19.

Ameyasema hayo alipokua akitoa ufafanuzi kuhusu umuhimu wa tozo na mikopo ya serikali katika kuleta maendeleo ya wananchi kwenye kazi za watanzania ambazo ni kilimo, uvuvi na ufugaji.

Rais Samia amesema pamoja na mikopo hiyo kusaidia uchumi wa nchi ila inasaidia pia mwananchi mmoja mmoja kwa sababu mzunguko wa fedha unasaidia kupunguza ukata wa wananchi.

“Kwa hiyo fedha hii pamoja na kusaidia uchumi wa nchi bado inasaidia mtu mmoja mmoja, sasa leo hii mtu aje aseme mama huyu anakopa kopa, mikopo mibaya haifai, serikali ya kukopa kopa toka tumepata uhuru na tulifika kipindi tukakopa sana hadi tukapelekwa kwenye adjustiment na tukafaulu na nchi inaendelea,” aliongeza Rais Samia.


Rais Samia ameendelea kusema, “Ndugu zangu, siku ile ya tarehe 19 march, wakati mnanitwika huu msalaba niliapa kwa Mungu na Mungu ananishuhudia,kwamba nitaleta maendeleo na kuimarisha ustawi wa watu, kuleta ustawi wa nchi hii sio kazi ndogo na hauji kwa miujiza, lazima utumie kila mbinu unayoweza kuitumia ili ustawi uje,”


“Kwa hiyo kama kuna Tozo tunaendelea kutozana na sisi sio wa kwanza, na kama kuna mikopo itasaidia basi tutakopa tu. Wala sitasema mikopo basi madhali inachafua watu. Tunaposema tulete maendeleo lazima mikopo iwepo.” Rais Samia.


“Wamenitizama nilivyo wakanijaribu, wamekosea hapa sipo. Lakini uzuri ni kuwa nilitoa ufafanuzi wa siku moja tu na wenye nchi wakaongea, na hicho ndicho kinachonipa nguvu za kuendelea.” Aliongeza

Kuhusiana na Tozo za serikali Rais Samia amesema ni lazima kukopa ili kuendelea kuongeza fedha kwa kuongezea kile kilichopo kwenye tozo.


“Takwimu zilizotolewa na mawaziri hapa zinatosheleza, kwamba pamoja na tozo ila mahitaji ya madarasa ni elfu 10, tumeweza mia tano kwa fedha ya tozo, tutafika lini? Lazima tukope…Mawaziri tupeni hizo takwimu haraka watu wajue inawezekana kweli hawajui kwa nini tunakopa.” Rais Samia.

Hivi karibuni kumekua na mijadala tofauti kwenye mitandao ya kijamii inayoongelea mikopo ya serikali na hatma ya nchi itakaposhindwa kulipa madeni hayo.

Watu 9 wahofiwa kufa maji Kisiwani Pemba
Eric Omondi atangaza kuvamia faragha za wasanii wa Kenya