Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amewasili jijini London, Uingereza kwa ajili ya kushiriki shughuli rasmi ya msiba wa Malkia Elizabeth II.

Viongozi mbalimbali walioalikwa akiwemo Rais Samia watatoa heshima zao za mwisho kwa Marehemu kwenye eneo la Westminster Hall ambapo pia atatia saini kitabu cha maombolezo.

Baada ya hatua hiyo Rais Samia atahudhuria hafla fupi ilioandaliwa Mfalme Charles III ambaye amemrithi mama yake Marehemu Malkia Elizabeth II.

Hafla hiyo ambayo pia imeandaliwa na Malkia Mfariji (Queen Consort), Camilla Parker Bowles itafanyika katika Kasri ya Buckingham jijini London.

Aidha, siku ya Jumatatu, Rais Samia atahudhuria Mazishi ya Kitaifa ya Malkia Elizabeth II yatakayofanyika kwenye Kanisa la Westminster Abbey, Mwili wa Malkia Elizabeth utalazwa kwenye kasri la Windsor.

Habari kuu kwenye magazeti ya leo Septemba 19, 2022
Rais wa Senegal arejesha wadhifa wa Waziri Mkuu