Umoja wa Watemi wa Kisukuma kwa kushirikiana na Umoja wa Machifu Tanzania umemsimika Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kuwa mkuu wa Machifu Tanzania na kumpa jina la Hangaya, lenye maana ya Nyota inayong’aa asubuhi.

Rais Samia amesimikwa kuwa mkuu wa Machifu wakati wa tamasha la Utamaduni wa Mtanzania ambalo limefikia kilele chake hii leo Septemba 8, wilayani Magu mkoani Mwanza,

Katibu wa Umoja wa Machifu wa Kisukuma, Mtemi Aaron Mikomangwa amesema wamemsimika Rais Samia kuwa mkuu wa Machifu Tanzania na jina hilo la Hangaya ikiwa ni kutambua mchango wa Serikali yake katika kuthamini na kusimamia utu wa wanyonge pamoja na utamaduni wa Mtanzania.

Lengo la tamasha hilo la Utamaduni wa Mtanzania lililoanza jana, ni kudumisha, kurithisha na kuutangaza Utamaduni wa makabila ya Tanzania.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, akivalishwa Mavazi ya Kimila kuwa  Chifu Mkuu wa Machifu wote Tanzania na kuitwa jina la Hangaya yani ni Nyota inayong`aa, katika Tamasha la Utamaduni (Mila na Desturi zetu) lililofanyika leo Sept,08,2021 katika Viwanja vya Redcross Kisesa Magu, Mkoani Mwanza.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, akivalishwa Mavazi ya Kimila kuwa  Chifu Mkuu wa Machifu wote Tanzania na kuitwa jina la Hangaya yani ni Nyota inayong’aa, katika Tamasha la Utamaduni (Mila na Desturi zetu) lililofanyika leo Sept,08,2021 katika Viwanja vya Redcross Kisesa Magu, Mkoani Mwanza.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, akipokea Mkuki na Ngao kutoka kwa Chifu Fundi Kira Makamu Mwenyekiti wa Umoja wa Machifu Tanzania mara baada ya kusimikwa kuwa Mkuu wa Machifu wote Tanzania na kuitwa jina la Hangaya yani Nyota inayong`aa, katika Tamasha la Utamaduni (Mila na Desturi zetu) lililofanyika leo Sept,08,2021 katika Viwanja vya Redcross Kisesa Magu, Mkoani Mwanza.
PICHA NA IKULU.

Mabingwa wamerejea kuibeba Young Africans Kimataifa
Bongo Zozo ampongeza Kocha Kim Paulsen