Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amekutana na kuzungumza na Mjumbe maalum wa Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson katika maswala ya Biashara kati ya Uingereza na Tanzania, Lord John Walney.

Walney amekutana na Rais Samia kujitambulisha akiwa na jukumu la kuwa kiungo kati ya nchi hizo mbili kuhusu masuala ya biashara na utalii nchini Tanzania.

Amesema kukutana kwake na Rais Samia kumempa fursa ya kujua vipaumbele vya Serikali ya Tanzania ambavyo vitamuwezesha kushawishi zaidi wafanyabiashara wa uingereza kuwekeza katika sekta hizo.

Kwa upande wake Rais Samia amemshukuru Walney kwa uamuzi wake wa kukutana nae na kujitambulisha kwake na kumueleza kuwa Serikali ya Tanzania ipo tayari kushirikiana na Uingereza.

Uingereza ni moja ya nchi ambazo zinaongoza kuwekeza nchini Tanzania, hivyo kupitia mjumbe huyo kutaongeza fursa zaidi na kukuza ushirikiano.

Madanguro Tanga marufuku.
Habari kubwa kwenye magazeti leo, Novemba 1, 2021