Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amemuagiza Naibu Waziri wa Afya Dkt Godwin Mollel kuangalia njia zote zinazowezekana kuhakikisha jengo la kutolea huduma za tiba ya saratani linakamili kwa haraka katika hospitala ya KCMC Moshi.

Rais Samia ameyasema hayo leo Oktoba 16, 2021 wakati akihutubia kwenye hafla ya maadhimisho ya Jubilee ya miaka 50 ya KCMC Moshi.

Amesema katika kuunga mkono juhudi za wataalamu wa afya, serikali inatekeleza ahadi yake ya kugharamia ujenzi wa jengo hilo kwa asilimia 100 ujenzi ambao utagharimu kiasi cha shilingi Bilioni 4.

“Hadi sasa bilioni moja imefika na bilioni nyingine moja inatarajiwa kuletwa,” Amesema Rais Samia.

Aidha Rais Samia amewahakikishia kwamba fedha za ujenzi wa jengo hilo zote zitapelekwa ili jengo likamilike kwa wakati na huduma zianze kutolewa kwa haraka.

Sambamab na hayo yote serikali imeendelea kuboresha miundombinu ya hospitali ya KCMC Moshi, ikiwa ni pamoja na kuwezeshwa kuwekwa mtambo wa kuzalisha hewa tiba (Oxygen) wenye thamani ya shilingi milioni 800 ambapo mtambo unauwezo wa kuzalisha mitungi 400 kwa saa 24.

Awali akiongea na wageni waalikwa Naibu waziri wa Afya na Mbunge wa Moshi Dk Godwin Molel amewapa moyo wahudumu wa Afya wa KCMC kwa kujituma pamoja na uchache wao huku akiwaasa waendelee kuwahudumia wananchi bila kuchoka kwa kuwa lengo la Serikali la kuongeza ajira Hospitalini hapo linafanyiwa kazi.

Hospitali ya KCMC inayosimamiwa na taasisi ya dini imekua ikihudumia kanda ya kaskazini kwa miongo 50 ikiwa na vitengo tofauti vya huduma za jamii kwa usimamizi wa serikali.

Biharamulo yaridhia kuhamia mkoa mpya wa Chato.
Miss Kiziwi Tanzania na Elimu ya Afya ya uzazi