Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amewaagiza mawaziri wa fedha na uchukuzi wa nchi zote mbili kushirikiana kwa ukaribu kutafuta fedha ili kuharakisha ujenzi wa reli ya Uvinza, Msongati hadi Gitega.

Ameyasema hayo wakati akihutubia kwenye ziara yake ya siku mbili nchini Burundi na kusema kuwa moja kati ya mambo waliyozungumza na mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Burundi Evariste Ndayeshimiye ni pamoja na uboreshaji wa miundombinu kama reli, barabara, na meli inayounganisha nchi zote mbili.

Amesema kuwa kwa kubresha miundombinu itasaidia wafanyabiashara kutumia fursa zaidi na kukuzu uchumi wa biashara katika nchi zote mbili.

Aidha Rais Samia ameelezea mikakati ya miundombinu na jinsi inavyoendelea ikiwemo ujenzi wa reli ya umeme ambao kwa sasa unaendelea kujengwa kuelekea Tabora hadi Kigoma kukutana na reli ya Msongati itakayounganisha na Burundi.

Hata hivyo pia Tanzania inafanya upanuzi wa Bandari ya Dar es Salaam, Kigoma, Kalema na Kabwe ambazo ni kiungo muhimu cha usafiri kati ya Tanzania na Burundi huku ukarabati wa meli ukiendelea, meli ya kubeba mafuta tani 350, pamoja na ujenzi wa meli mpya mbili moja ya kubeba abiria 400 na mizigo tani 600 na nyingine niyakubeba mizigo peke yake tani 2800.

Halikadhalika Rais Samia amewahasa wafanyabiashara wa Burundi kuendelea kutumia bandari za Tanzania na kusisitiza kuwa Tanznania iko tayari kuboresha miundombinu ya usafiri na usafirishajiili kazi zifanyike kwa haraka zaidi.

Sambamba na hayo yote Tanzania imetanga hekta 10 zenye mita mraba 10,000 kwaajili ya Burundi baada ya ombi la Rais Evariste la kuomba ardhi nchini Tanzania

Hadithi za 'MAGWIJI' zinafanana
Kwa nini Niyonzima na sio wengine? Ufafanuzi watolewa