Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akiwa ziarani Manyara ametembelea na Hospital ya Rufaa ya mkoa wa Manyara na kuwajulia hali wagonjwa wanaopatiwa matibabu katika hospital hiyo.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akiwa na Naibu Waziri wa Afya, Dkt. Godwin Mollel wakati akimsikiliza Mganga Mfawidhi wa Hospitali Rufaa ya Mkoa wa Manyara, Dkt. Catherine Magali akielezea maendeleo ya Ujenzi wa Hospitali hiyo Babati.

Rais Samia amewatembelea wagonjwa hao hii leo Novemba 23, 2022 ikiwa ni muendelezo na hitimisho la ziara yake ya kikazi kwa siku mbili Mkoani Manyara ya kukagua na kuzindua miradi mbalimbali ya kimaendeleo.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akiwajulia hali Wagonjwa wanaopatiwa matibabu katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Manyara iliyopo Babati katika ziara yake ya siku mbili Mkoani humo.

Akiwa na Naibu Waziri wa Afya Dkt. Godwin Mollel wamekagua maendeleo ya ujenzi wa Hospitali ya Babati Mkoani Manyara kwa usaidizi wa mganga mfawidhi wa Hospitali Rufaa ya Mkoa wa Manyara, Dkt. Catherine Magali.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM Taifa akiwasalimia Wananchi mara baada ya kukagua maendeleo ya Ujenzi wa Ofisi za chama, Babati Mkoani Manyara.

Aidha, Rais Samia pia amezindua barabara za Mitaa za Mji wa Babati kilometa 8.1 na kuahidi kujenga bararaba ya lami ya kilometa tano zaidi katika Mji huo.

Rais Samia Suluhu Hassan katika picha ya pamoja na viongozi wa Chama hii leo Novemba 23, 2022.

Adebayor: Natamani kuwa sehemu ya Simba SC
Young Africans yamnyima usingizi Allan Okello