Rais Samia Suluhu Hassan amewataka wakuu wa wilaya kufanya kazi kwa weledi na kuacha kusubiri mkeka wa uteuzi na kuwataka wakuu wa mikoa kusimamia utendaji kazi wa viongozi wa wilaya kwa kuwasilisha ripoti.

Rais Samia ameyasema hayo katika hafla ya utiaji saini Mkataba wa Usimamiaji wa Shughuli za Lishe leo Septemba 30, 2022 jijini Dodoma.

“Nasikia hamfanyi kazi mnasubiri mkeka napata mesage, malizia huku hawafanyi kazi wako kama wamepigwa ganzi. nikute mkuu wa wilaya kapigwa gazi, nikute kapigwa gazi! nilisema tulichokifanya ni performance ya utendaji wenu,” amesema Rais Samia.

“Sikusema nitawabadilisha leo na kesho nimesema tumefanya perfomance tumejua nani mzuri nani mbaya aliyesema nataka kuwabadilisha nani? kama wabaya nilitaka kuwatia kwenye mafunzo niwarekebishe, kwahiyo kama hamfanyi kazi hao ndio wangu,” amesema Rais Samia.

“Wakuu wa wilaya nchi nzima fanyeni kazi zenu, kutoa mkeka ni kazi yangu na nitatoa wakati ninapoona muafaka sasa hivi kwenu ni kufanya kazi,”

“Wakuu wa mikoa nataka ripoti za wakuu wenu wa wilaya aliyepigwa gazi nani, mwenye nusu kaputi nani kama hawawezi tutoe tuweke wengine nataka ripoti za wakuu wenu wa wilaya na hili tutalizungumza jioni leo,” ameongeza Rais Samia

Safari zisizo lazima zisitishwe kuepuka Ebola
Rais Samia ahofia vijana kukosa nguvu za kiume