Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ametengua uteuzi wa Mkuu wa Wilaya na Mkurugenzi wa halmashauri ya Morogoro, ambako wafanyabiashara wadogo waliondolewa kwa nguvu hivi karibuni.

Rais Samia ametangaza uamuzi huo leo Juni 15, 2021 mkoani Mwanza wakati wa mkutano wake na Vijana wa Tanzania kupitia vijana wa mkoa huo.

Amesema amesikitishwa na kitendo cha kuondolewa kwa nguvu kwa wafanyabiashara hao, na kwamba kama ingekuwa ni lazima wafanyabiashara hao kuondolewa ingetumika njia nyingine na si nguvu na kuharibu bidhaa zao.

Aidha, amemuagiza Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Ummy Mwalimu kusimamia jambo hilo.

Kwa mujibu wa Rais Samia  wafanyabiashara hao walitengewa eneo la mbali kwa ajili ya  kufanya biashara zao na walipoona hakuna biashara waliamua kurudi maeneo ya mjini na ndipo walipoanza kuondolewa kwa nguvu.

Mavunde: Tunawatesa watanzania kwa riba kubwa
Marekani yapiga marufuku uingizwaji wa mbwa