Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amewatunuku Kamisheni Maafisa Wanafunzi Kundi la 03/19 – Shahada ya Sayansi ya Kijeshi na Kundi la 69/21 Refu Pamoja na Mahafali ya tatu ya Shahada ya Sayansi ya Kijeshi Kundi la 03/19.

Rais Samia amewatukutu Maafisa Kamisheni hizo hii leo Novemba 26, 2022 katika Chuo cha Mafunzo ya Kijeshi (TMA), Monduli Mkoani Arusha na kukishukuru Chuo cha Uhasibu Arusha kwa kushirikiana na Jeshi kufanikisha utoaji wa mafunzo kwa maafisa hao huku akiwapongeza wahitimi wa mafunzo hayo ya kijeshi.

Amesema, “Ndugu zangu napenda kukishukuru Chuo cha Uhasibu Arusha kwa kushirikiana na Jeshi kufanikisha utoaji wa mafunzo haya kwa wanajeshi wetu yanayohakikisha wanakuwa na utaalamu na pia nawapongeza wahitimu wote wa mafunzo haya ya kijeshi.”

Mara baada ya hotuba hiyo, kutunuku na pongezi kwa wahitimu, Rais Samia pia alivunja Mahafali hayo ya tatu ya Shahada ya Sayansi ya Kijeshi kati ya Chuo cha Mafunzo ya Kijeshi Monduli na Chuo cha Uhasibu Arusha.

Polisi watatu wauawa kwenye msafara, Kiongozi atekwa
Tanzania mjumbe Kamati kuu Wanyamapori, Mimea