Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amezindua kitabu cha mwanamuziki nguli wa Hip Hop, Mr 2 Proud, maarufu kama Sugu kiitwacho muziki na maisha kwenye tamasha la kutimiza miaka 30 katika tasnia ya muziki.

Rais amemtunukia tuzo, Sugu na akimpongeza kuwa miongoni mwa wasanii wenye nyimbo zenye maadili.

Tamasha hili limepambwa na burudani kutoka kwa wasanii mbalimbali ikiwa ni pamoja na Sugu mwenyewe ambaye ametumbuiza na kukonga nyoyo za mamia ya watu waliohudhuria.

Tamasha hilo lililoitwa The dream concert, Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mohamed Mchengerwa, Katibu Mkuu. Dkt, Hassan Abbasi, Naibu Katibu Mkuu, Saidi Yakubu, watendaji wa Wizara na wadau mbalimbali wamehudhuria.

Habari kuu kwenye magazeti ya leo June 1, 2022   
Amazulu yampa ofa nono Kocha Pablo, Orlando, Raja Casablanca zatajwa