Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan leo Agosti 28,2021 amezindua miradi mbalimbali ya maendeleo Kizimkazi, Zanzibar katika kilele cha Tamasha la Kizimkazi.

Aidha Rais Samia amezindua ukarabati wa madarasa ya chekechea na ofisi za walimu, Nyumba za madaktari na jengo la ofisi ya maendeleo, pia amepokea gari la kubebea wagonjwa katika Wilaya ya Kusini, Mkoa wa Kusini Unguja  .

Pamoja na uzinduzi huo Rais Samia ameongozana na raia wa kigeni kutoka nchi mbalimbali duniani wakiwa na lengo la kutembelea maeneo yenye vivutio vya kitalii visiwani Zanzibar na kwenda kutangaza katika nchi zao.

Hata hivyo Rais Samia amewasisitiza wananchi wa Zanzibar kuendelea kujikinga na maradhi ya COVID 19 na kuwakumbusha kushiriki katika sensa ya watu na makazi ambayo inatarajiwa kufanyika mwakani 2022.

Tamasha la Kizimkazi lina lengo la kuendeleza tamaduni za Wanzanzibari, kuhamasisha shughuli za maendeleo, na Kutangaza fursa za kiuchumi kama kilimo, utalii, na uvuvi.

Leo Agosti 28, 2021 imekua kilele cha Tamasha la Kizimkazi ambalo limedumu kwa wiki moja kwa kushirikisha mafunzo ya wajasiriamali, utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo, sanaa, tamaduni na michezo ikiwa ni pamoja kuendelea kutoa chanjo ya COVID 19.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, akikata utepe kuzindua rasmi Jengo la Ofisi ya Maendeleo Kizimkazi iliyojengwa kwa ufadhili wa Benki ya CRDB leo Agosti 28,2021 kwenye Tamasha la Kizimkazi zilizofanyika leo tarehe 28 Agosti 2021 katika Kijiji cha Kizimkazi Mkoa wa Kusini Unguja.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, akikata utepe kuzindua rasmi Skuli ya maandalizi Kizimkazi katika Tamasha la Kizimkazi Sherehe ya Siku ya Wakizimkazi zilizofanyika leo tarehe 28 Agosti 2021 katika Kijiji cha Kizimkazi Mkoa wa Kusini Unguja.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, akikata utepe kwa ajili ya kupokea rasmi Ambules iliyotolewa kwa ufadhili wa Benki ya NBC kwa ajili ya kutoa huduma katika Kijiji cha Kizimkazi kwenye Tamasha la Kizimkazi lililofanyika tarehe 28 Agosti 2021 katika Kijiji cha Kizimkazi Mkoa wa Kusini Unguja
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, akiondoa kitambaa kuzindua rasmi Nyumba za Madaktari na Jengo la Ofisi ya Maendeleo Kizimkazi katika Tamsha la Kizimkazi zilililofanyika leo tarehe 28 Agosti 2021 katika Kijiji cha Kizimkazi Mkoa wa Kusini Unguja.

Habari kubwa kwenye magazeti leo, Augusti 29, 2021
Koffi Olomide awasili kutumbuiza wiki ya mwananchi