Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amefanya mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Mafuta ya Taifa, ya Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) ENOC LLC, Saif Al Falasi aliyeambatana na ujumbe wake.

Rais Samia amekutana ujumbe huo hii leo Januari 28, 2023 Ikulu Jijini Dar es Salaam ambapo tayari Serikali kupitia Wizara ya Nishati Januari 27, 2023 kusaini mkataba wa makubaliano (Memorandum of Understanding), na Kampuni hiyo kuhusu Ujenzi wa Kitovu cha Mafuta (Fuel Hub), hapa nchini.

Waziri wa Nishati, Januari Makamba alisema Tanzania itaanza kuhifadhi akiba ya mafuta yatakayotumika katika kipindi cha zaidi ya miezi mitatu, tofauti na sasa ambapo inahifadhi kwa mujibu wa sheria kwa siku 15 pekee.

Alisema, ujio wa kampuni hiyo, utasaidia kuboresha miundombinu ya bomba la kushusha mafuta bandarini na uhifadhi wa mafuta ya kutosha nchini.

Mabalozi wa Ulaya waikubali miradi ya FETA
Mpango awataka Wanazuoni kuipaisha Tanzania uandishi wa Vitabu