Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan anatarajia kufanya ziara ya kiserikali ya siku mbili nchini Rwanda kuanzia Agosti 2, 2021 kwa mwaliko rasmi wa wa Rais wa nchi hiyo, Paul Kagame

Akiwa Nchini Rwanda Rais Samia anatarajiwa kufanya mazungumzo rasmi na mwenyeji wake, kisha atashuhudia utiaji saini hati za makubaliano na kuzungumza na vyombo vya habari

Kwa mujibu wa wa taarifa iliyotolewa na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais Ikulu imeeleza kuwa ziara hiyo ya siku mbili inalenga kuimarisha zaidi uhusiano na ushirikiano baina ya Rwanda na Tanzania.

Tanzania kupata chanjo milioni 11 - Msigwa
Naibu waziri balozi Mbarouk azindua safari ya baiskeli ya 'GREAT AFRICAN CYCLING SAFARI'