Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, ni sehemu ya viongozi wa nchi waalikwa katika sherehe za kuapishwa kwa Rais Mteule wa Zambia Hakainde Hichilema zinazoendelea mjini Lusaka.
 
Sherehe za kuapishwa kwa Rais huyo Mteule wa 7 wa Zambia zinafanyika, baada ya wananchi wa Zambia kushiriki kwa amani na utulivu katika zoezi la uchaguzi mkuu uliofanyika mwanzoni mwa mwezi huu.
 
Rais Samia ameongozana na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk, Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Shaka Hamdu Shaka, Katibu wa Idara ya Oganaizesheni ya CCM Maudline Cyrus Castico na Waziri Mkuu Mstaafu na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Mizengo Pinda.
 
Wengine ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Kombo Hassan Juma, Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Tanga na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM – Henry Shekifu na Mbunge wa Jimbo la Mtera na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Livingstone Lusinde.
 
Aidha, Rais mstaafu wa awamu ya nne Dkt. Jakaya Kikwete naye anashiriki katika sherehe hizo akiwa kiongozi wa timu ya waangalizi wa uchaguzi mkuu uliofanyika nchini Zambia kutoka Jumuiya ya Madola.

Gwajima, Silaa watemwa ujumbe kamati ya Bunge
Mwanafunzi ajinyonga baada ya kusimamishwa masomo