Wananchi wa kata ya Majengo Tunduma wamekusanya fedha na kuanza ujenzi wa shule mpya ya msingi ambayo wanampango wa kuita shule ya mama Samia Hassan Suluhu ambaye ni Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kutambua mchango wake katika jimbo hilo.

Hayo yamesemwa na Diwani wa kata hiyo Frank Mponzi wakati wa ziara ya kikazi ya Naibu Waziri wa TAMISEMI na mbunge wa jimbo la Tunduma, David Silinde.

Aidha wananchi hao wamesema kuwa wameamua kujenga shule mpya ya msingi kutokana watoto wengi hutembea umbali mrefu kwenda shule hivyo shule hiyo itawarahisishia watoto hao kusoma.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Mji wa Tunduma Regina Bieda, amesema kwasasa wamewaingizia milioni 10 kuanza ujenzi huo baada ya Wananchi kufyatua matofali elfu sabini tano na kuwa na eneo hivyo ujenzi huo utaanza mda wowote na ifikapo januari 2022 shule hiyo itaanza kutoa huduma.

Kwa upande wake Naibu Waziri wa TAMISEMI David Silinde amesema ujenzi wa shule hiyo ya msingi ya mama Samia wao kama serikali watajibu hilo kwa kutafuta fedha ili shule hiyo ikamilike maana hata Rais akisikia atafurahi kuona wananchi wameipa shule jina lake.

Aidha Naibu Waziri wa TAMISEMI David Silinde amelizishwa na kasi ya ujenzi wa shule hiyo.

Rais Mwinyi: Uwajibikaji ni tatizo kwa watumishi wa Serikali
Sababu za Tasisi za kidini kutolipa kodi