Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kupata chanjo ya Covid 19 ya Johnson & Johnson iliyowasili nchini Julai 24.

Tukio hilo litafanyika ikiwa ni sehemu ya uzinduzi wa chanjo hiyo ambayo itaanza kutolewa kwa makundi maalum wakiwemo wazee, wagonjwa, wahudumu wa sekta ya afya na makundi ya mstari wa mbele.

Taarifa iliyotolewa na Waziri wa Afya, Dk Dorothy Gwajima, baada ya Rais kuchanjwa katika hafla ya uzinduzi itakayofanyika ikulu Julai 28, taratibu za kutoa chanjo kwenye vituo vilivyoandaliwa zitaanza.

Julai 24 mwaka huu Dk Gwajima aliongoza mapokezi ya chanjo hiyo hiyo ambayo ilikuja dozi 1,058,400 ikiwa ni shehena ya awamu ya kwanza, serikali ya Tanzania ilijiunga na mpango wa Covax facility kwa ajili ya kupata chanjo hiyo Juni 15 mwaka huu

Serikali yatoa tamko miamala kutolewa
Makamba: Ni hatari kupotosha watu