Rais wa Jmhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan na miongoni mwa baadhi ya wakuu wa nchi ambao wametumia usafiri wa pamoja wa basi, kuelekea katika eneo la Westminster Abbey yanapofanyika mazisi ya Malkia Elizabeth II hii leo septemba 19, 2022.

Viongozi wengine waliohudhuria mazishi hayo ni pamoja na Rais wa Kenya, William Rutto aliyeambatana na mkewe Rachel  na Naibu Waziri wa Mambo ya nje na Ushirikiano wa Afrika mashariki wa Tanzania Mbarouk Nassor Mbarouk.

Mazishi hayo yamehudhuriwa na  takriban watu 2,000, wakiwemo viongozi 500 kutoka Ulaya na viongozi wa mataifa wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Madola. 

Rais Samia Suluhu Hassan (watatu kulia), na Rais wa Kenya, William Ruto (wapili kushoto) katika usafiri wa pamoja kuhudhuria mazishi ya Malkia Elizabeth II nchini Uingereza.

Wageni wengi waliohudhuria mazishi ya Malkia Elizabeth II, walitakiwa kutumia usafiri wa pamoja ambapo ripoti zinaonyesha kuwa Rais wa Marekani Joe Biden ni miongoni mwa viongozi wachache ambao wameruhusiwa kutumia helikopta yake jijini London. 

Wakuu wa Nchi waliohudhuria mazishi hayo, walikuwa wamehimizwa kusafiri kwa ndege za kibiashara ili kuepuka msongamano mkubwa kwenye viwanja vya ndege vya London.

Serikali yatenga Bil. 3 ujenzi Hospitali ya rufaa
Umeme Kigoma: Serikali kuokoa Bil 22.4