Rais wa Jamhri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amepokea Kombe la Ushindi la Michuano ya Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati kwa Vijana wenye Umri chini ya Miaka 23 (CECAFA Challenge Cup 2021) viwanja vya Ikulu, Jijini Dar es Salaam.

Aidha Rais Samia amewataka wananmichezo kupata chanjo za virusi vya corona zinasaidia maumivu na hatari ya vifo kwa watu ambapo amesema kuwa yeye kama mkuu wa nchi hawezi kuipeleka jamii yake kwenye hatari.

“Suala la chanjo ya Covid-19 ni muhimu, na wanamichezo kama hamjachanjwa naomba mkafanye, kwa kuwa mnasafiri sana, mimi Mama yenu, mkuu wenu, sitapeleka jamii yangu kwenye hatari, huwezi kushindana na mwanadamu mwenye kinywa, lakini ukweli ni kwamba chanjo hizi zinasaidia’ amesema Rais Samia

“Nimefurahia kupokea Kombe hili la CECAFA (U23) tunaamini kwamba kila safari huanza na hatua moja naamini ni safari ya kwenda kuchukua makombe mengine makubwa mbele ya safari ikiwa tu vijana hawa tutawatunza lakini ikiwa tutawaacha waende nyumbani Tukiwahitaji waje, hatutofika”amesema Rais Samia 

Rais wa zamani wa Bolivia ataka kujiua jela
TANROAD yatoa onyo wanaotupa taka barabarani