Rais wa shirikisho la soka nchini Armenia Ruben Hayrapetya amechukizwa na mwenendo wa kiungo mshambuliaji Henrikh Mkhitaryan, ambaye amekua na wakati mgumu wa kucheza kila mwishoni mwa juma tangu alipojiunga na Man utd wakati wa majira ya kiangazi.

Mkhitaryan alijiunga na mashetani wekundu akitokea Borussia Dortmund kwa ada ya uhamisho wa Pauni milioni 26, na alitarajiwa kuwa sehemu ya kikosi cha kwanza cha Jose Mourinho, lakini imekua tofauti.

Mpaka sasa kiungo huyo mwenye umri wa miaka 27, ameshacheza kwa dakika 104 za michezo ya ligi ya nchini England.

“Sifahamu kitu gani ambacho meneja wa Man Utd anakifikiria juu ya Mkhitaryan, lakini ukweli ni kwamba hatufurahishwi na mwenenedo uliopo,” Hayrapetyan aliwaeleza waandishi wa habari wa nchini Armenia.

“Nimekua na mawasiliano na Mkhitaryan, lakini hata kwa upande wake hafahamu nini ambacho Jose Mourinho anakifikiria dhidi yake.

“Mkhitaryan amekua akifanya mazoezi na anaendelea vizuri, na kila mmoja kati yetu anafahamu kiwango chake cha soka, lakini bado tunakosa jibu sahihi kwa nini hachezi.”

Historia Ya Soka La Wanawake Kuandikwa Kesho
Manara: Sisi Hatuna Presha Na Hata MO Hana Presha