Rais wa Brazil, Michael Temer ameburuzwa mahakamani kwa tuhuma za kupokea rushwa huku rais huyo akikana tuhuma hizo.

Aidha, mwendesha mashtaka wa nchi hiyo amesema kuwa rais huyo anakabiliwa na tuhuma nyingi tofauti na za ufisadi.

Temer ametupilia mbali maoni na wito unatolewa na jumuiya ya kimataifa wa kumtaka kujiuzulu kutokana na tuhuma zinazomkabili.

Hata hivyo, mahakama nchini humo ndiyo pekee itakayoamua kama kesi hiyo ipelekwe katika bunge la uwakilishi ili kupigiwa kura ya kumuondolea mashtaka ama kuendelea nayo.

 

Chanzo Kuvunjika Daraja la Matrilioni la Sigiri Kenya Chazua Utata
Lowassa kuhojiwa na polisi leo