Kamati ya bunge la Brazil jana imepiga kura kupinga hatua ya kuwasilishwa kesi ya madai ya rushwa yanayomkabili Rais wa nchi hiyo, Michel Temer kufikishwa mahakama ya juu zaidi ili kiongozi huyo afunguliwe mashtaka.

Kura hiyo haina nguvu kisheria, na bunge zima litazimika kupiga kura dhidi ya madai hayo, ambayo yanaweza kuidhinishwa iwapo tu theluthi mbili ya wabunge watapiga kura hiyo ya maamuzi.

Rais huyo wa Brazil alifunguliwa mashtaka mwezi uliopita akihusishwa na njama za matumizi mabaya ya fedha za umma, yanayohusisha kampuni kubwa duniani ya kusindika nyama, JBS.

Aidha, Mwendesha mashtaka mkuu wa Serikali wa nchi hiyo, Rodrigo Janot alimtuhumu Temer kwa kuratibu mpango wa kupokea rushwa ya kiasi cha Dola Milioni 11.85 kutoka JBS, katika miezi tisa iliyopita.

Vile vile, Bunge zima litapiga kura tena Agosti 2, ikiwa ni baada ya wiki mbili za mapumziko ingawa uungwaji mkono wa Temer unazidi kupungua lakini bado anaamini kwa kiasi kikubwa kushinda kishindo hicho cha kura ya bunge zima.

Hata hivyo, mwendesha mashtaka, Janot amesema kuwa anatarajia kuwasilisha mashtaka mawili mapya ya wizi wa mali ya umma dhidi ya Temer katika kipindi cha wiki chache zijazo.

Hatua hiyo ya kamati ya bunge inachukuliwa kama ishara ya ushindi kwa Temer ikiwa ni siku moja baada ya rais wa zamani wa nchi hiyo, Lula da Silva kuhukumiwa kifungo cha miaka 9 kwa mashitaka ya matumizi mabaya ya mali ya umma.

Chadema watinga Takukuru, wahoji madiwani wao saba kujivua uanachama
Video: Gonjwa la tumbo lamvuruga Sethi wa Escrow Keko, Siri mauaji Chadema yafichuka