Hafla ya kumuaga aliyekuwa Rais wa Chad inafanyika leo Aprili 23, 2021 katika Mji Mkuu N’Djamena kabla ya mazishi yake katika mji aliozaliwa wa Berdoba.

Aidha sala maalum itafanyika katika Msikiti Mkuu wa Mji wa N’Djamena, ambapo mida ya alasiri mwili wake utasafirishwa na kupelekwa mji aliozaliwa wa Berdoba, takribani kilomita 1000 kutoka Mji Mkuu wa nchi hiyo kwa ajili ya mazishi.

Hata hivyo, waasi waliokuwa wanapambana na Rais Idris wametoa tahadhari kwa marais wa mataifa mengine kutokuhudhuria mazishi hayo kwa usalama wao.

Licha ya hilo, bado inatarajiwa marais wa mataifa mengine kuhudhuria mazishi ya Rais huyo kutokana na mchango wake unaotambulika katika kupambana na waasi ukanda wa Magharibi mwa Afrika.

Baraza la kijeshi linaloongozwa na mwanae Jenerali Muhamad Idris Deby lilichukua uongozi wa nchi hiyo mara baada ya kifo cha Rais, na kwa sasa anaungwa mkono na wakuu wa kijeshi na serikali ya Ufaransa, ambapo jeshi litaongoza nchi kwa miezi 18 kabla ya kufanyika kwa uchaguzi.

Viongozi wa upinzani wanalaani uongozi wa jeshi hilo na kuuita ni mapinduzi ya nchi, pia Jenerali mmoja wa jeshi hilo pia ameonyesha kupinga maamuzi ya Baraza hilo la mpito.

Vyanzo vya habari vinasema kuwa waasi hao wapo umbali wa kilomita 300 kutoka Mji Mkuu wa Nchi hiyo na wataalamu wanasema huenda waasi hao wakafanya mashambulio mengine.

Idris Deby alifariki Aprili 19, 2021 wakati akiongoza Jeshi katika mapambano dhidi ya waasi.

Aweso awataka Wahandisi, Wakandarasi kukaa mguu sawa
Samia ataka kila mtu kulinda afya yake